Mambo Sita Unayopaswa Kufahamu Kuhusu FORSAGE Kabla ya Kuwekeza Fedha Zako

Share on facebook
Share on whatsapp
Share on twitter
Share on linkedin

TAKE AWAY: Twenty years ago, it was a big deal when schools got their first computers. Today, it’s a big deal when students get their own laptops 👌 👨‍🎓👩‍🎓

Yapata usiku wa manane napigiwa simu na mtu ambaye hakuwa na shaka. Alijua kwa vyovyote nitapokea simu yake endapo nitaiona. Nikweli hakukosea. Simu haikuwa mbali sana na sehemu niliyokuwa nimelala baada ya uchovu wa siku nzima. Kiufupi nilikuwa nayo kitandani baada ya kupitiwa na usingizi.

Nilishtuliwa na simu na kujiuliza, ni nani ananipigia simu? Kwa kuwa taa ilikuwa inawaka, sikupata shida ya kufungua macho na kumtambua aliyekuwa ananipigia. Haraka haraka niliipokea na kumsalimia, akaniitikia “Marahaba”, na kunitaka radhi ya kunipigia simu usiku wa manane. Sikuwa na shida na hilo kwa maana mwili ulihisi kuchangamka kupokea simu yake.

Akaanza kunieleza sababu ya kunipigia na kisha kuanza kuniuliza maswali machache ya ufahamu juu ya kile alichotaka tushauriane. Huku nikisikiliza kwa umakini na kujibu kwa ufupi yale maswali, nikaanza kutambua kwamba FURSA ya kibiashara aliyoelezwa kuhusu Forsage pia ilimnyima usingizi.

Wale ambao waliwahi kuhudhuria semina za biashara ya mtandao ya mtandao, a.k.a Network Marketing, cryptocurrency, n.k… watakuwa wanaelewa jinsi mtu unavyokuwaga baada ya kuchomwa sindano za mafanikio makalioni. Zikikuingia sawa sawa, usingizi huwa unakata 😂😂🤣

Ok. Hebu turudi kwenye mada.
Baada ya kumsikiliza na kushauriana mawili, matatu, niliomba anipe nafasi niweze kufanya upembuzi yakinifu juu ya hii kampuni ya Forsage na hivyo nilianza kazi mara moja.

Kazi ambayo nimeifanya kwa kufanya marejeo kutoka katika vyanzo mbali mbali vinavyoaminika nikiongozwa na ufahamu wangu juu ya mifumo ya biashara ya kimtandao. Kwa hiyo, nakualika pia unaposoma matokeo ya utafiti huu… weka pembeni mapenzi au chuki dhidi ya mifumo hii ili uweze kufikia maamuzi yaliyo sahihi katika safari yako mpya.

Katika utafiti wangu, nilijikita kutafuta majibu ya maswali sita ambayo kwa leo nitayatolea majibu na kufanya hitimisho;-

  1. Forsage Ni Nini?
  2. Forsage Inafanyaje Kazi?
  3. Jinsi ya Kutengeneza Kipato Ukiwa na Forsage
  4. Siri ya Wanaotengeneza Kipato Kikubwa Ndani ya Forsage
  5. Mtiririko wa Mawasiliano ya Forsage
  6. Je, Forsage ni Halali?
  7. Hitimisho.

Twende kazi…

Haraka haraka, niligundua kwamba Forsage imejipatia umaarufu mkubwa sana nchini Nigeria ukilinganisha na nchi nyingine barani Afrika. Hapa nchini Tanzania, haijashika kasi sana pengine kwa sababu bado ni changa ki-umri.

Forsage ni Nini?

Forsage ni jukwaa lililojengwa kwa kutumia teknolojia mahiri ya kisasa na kandarasi inayoruhusu watumiaji kujihusisha moja kwa moja katika miamala ya kibinafsi na ya kibiashara.

Lilirushwa rasmi mnamo February 6, 2020 ndani ya Ethereum Blockchain.

Mwanzoni, waasisi wa mtando huu hawakujulikana kabisa. Lakini ilipofika July 1, 2020 serikali ya Ufilipino kupitia kitengo chake cha Security and Exchange Commission (SEC) ilifunua kwa uwazi katika ripoti yake ya ONYO na MARUFUKU kwamba kijana wa Kirusi ajulikanae kama LADO OKHOTNIKOV ndiye mwanzilishi na mmliki wa Forsage.

LADO OKHOTNIKOV – The Founder & CEO of Forsage

Forsage inalenga kuwasaidia watumiaji kujilimbikizia Ethereum (ETH). Unapotembelea tovuti ya Forsage, kuna uwezekano mkubwa wa kunaswa kirahisi. Hizi hapa ni baadhi ya promise:

Pia, kutoka kwenye tovuti, tumefanywa kuamini kuwa Forsage ni program ya Matrix Cycler. Lakini kwa ufahamu wangu mimi, Forsage ni pyramid scheme iliyounganishwa pamoja na Ethereum blockchain. Hakuna jipya!

Naweza nisiwe nimeelewa vizuri, lakini usijali. Nitafafanua…

Ni Nini Hasa Matrix Cycler Program?

Program ya Matrix Cycler ni mfumo (model) wa kibiashara unaotumiwa na baadhi ya wauzaji na wanunuzi wa bidhaa au huduma. Kwamba, badala ya kutumia fedha kutangaza bidhaa katika vyombo vya habari… fedha hizo hupewa watu ambao kwa dhamira na fahamu sahihi, wamejipa jukumu la kuambizana na hukuwa wao wakiwa wateja namba moja wa bidhaa husika.

Mara nyingi, katika program ya Matrix Cycler… mtu hufikia kigezo cha kuanza kulipwa anapokuwa ameleta wateja watano (5). Kila mmoja utembea na utaribu huo huo na hakuna kikomo cha wateja.

Nyingi ya program za Matrix Cycler ziko-hosted kwenye mtandao wa intaneti lakini tofauti na hii ya Forsage, iko hosted kwenye Ethereum Blockchain.

Katika ufafanuzi wangu hapo juu, umeona kwamba, ‘Matrix Cycler Program’ inahusisha transactions (miamala) kati ya bidhaa au huduma.

Sasa, ni tofauti na jinsi inavyofanyika kwenye Matrices za Forsage. Hakuna miamala ya ndani inayofanyika ndani ya jukwaa la Forsage. Na HAWANA bidhaa wala huduma yenye kuongeza thamani katika jukwaa hilo.

Badala yake, watumiaji wa jukwaa la Forsage wananunua ETH kwa kutumia fedha zao ili muamala upate kukamilika. Baada ya hapa wanatakiwa kununua cheo (position) ndani ya Matrices za Forsage kwa kutumia ETH. Na kisha usubiria nyongeza ya bonus ya nyongeza ya ETH zitokanazo na faida ya kupanda kwa ETH.

Lakini pia, wakati huo huo wakisubiri kupanda kwa thamani ya ETH ili waje wavune faida, wanapata nyongeza ya ETH zitokanazo nawatu wapya wanaojiunga chini yao.

Forsage Inafanyaje Kazi?

Ili uweze kuwa mawanachama hai wa Forsage unahitajika kuwa na mambo yafuatayo;-

  1. ETH Wallet
  2. Upline
  3. Downline

ETH Wallet ni mahali ambapo ETH unazopata kwenye platform zitakuwa zikitumwa.

Pia, unapofanya miamala kwenye jukwaa la Forsage, ETH Walllet yako itaongezeka.

Upline ni mtu au kiongozi wako aliyekutambulisha kwa mara ya kwanza ujiunge na Forsage. Wakati wa kujisajili, unatakiwa uingine ID namba ya upline wako.

Dowline inaamanisha watu wa chini yako. Kwa lugha nyingine, watu uliyowatambulisha Forsage na kujiunga chini yako.

Kadri unavyokuwa na idadi kubwa ya Downline, ndivyo unavyotengeneza kipato kikubwa. Na pia ndivyo Upline wako anavyozidi kutengeneza faida kubwa.

Mchakato wake…

Kwanza kabisa, inakupasa aida ku-install Trust Wallet katika simu yako au Metamask Wallet katika computer yako.

Kisha baada ya hapo unahitajika kuweka Ethereum katika Wallet yako. Baada ya hatua hizo, sasa unaweza kujisajili na Forsage kwa 0.05ETH.

Digit

Digit

At Digit, we strive to provide a flexible, affordable online high school to students of all types – whether you want an alternative to your brick-and-mortar school, need to make up credits to graduate, or have been out of school for awhile. Our Mission is to empower students to achieve their aspirations through flexible, convenient, affordable, and highly relevant educational programs.

We hope you enjoy reading this blog post.

Share on facebook
Share on whatsapp
Share on twitter
Share on linkedin
Leave a Replay

Why Digit?

You can make up credits without going to summer school, get ahead or immerse yourself in career fields as a test drive for college. Because our teachers are accredited, our courses carry the same unit value as in schools, you’ll be able to pass ACSEE exams.

Whatever your reason is for taking individual courses, we have the perfect class for you.

Recent Posts

Follow Us

Get Digit’s future articles in your inbox!

Get our latest articles delivered to your email inbox and get the FREE Higher Education Industry Report (40 pages, 50+ charts)!